Gazeti
la Tanzania Daima lemieripoti kuwa Serikali imeanza uhakiki wa vyeti
vya ndoa kwa watumishi wa umma. Hatua hiyo ambayo imewashtua watumishi
wengi wa umma, imeelezwa kuwa ni mwendelezo wa harakati za Serikali ya
Rais John Magufuli kuhakiki watumishi wa umma ili kuondokana na
watumishi hewa.
Wakati
Serikali ikianza na uhakiki wa vyeti vya ndoa, kazi ya uhakiki wa
watumishi hewa na vyeti vyao vya elimu inaendelea sehemu mbalimbali
nchini.
Kwa muhibu
wa Gazeti la Tanzania Daima habari ambazo limezipata zinasema kuwa
serikali imeanzisha uhakiki huo nchi nzima kwa madai kuwa baadhi ya
watumishi wa umma wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwamba wana ndoa ili
kupata nauli na stahiki zingine za likizo wakati hawana ndoa.
Habari
zaidi zinasema kuwa walimu wakuu wa shule zote za Wilaya ya Ilala
wamepewa siku mbili kutekeleza agizo hilo kwa walimu wao. Mmoja wa
walimu hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alilithibitishia
Tanzania daima kuwa ametoa siku mbili kwa walimu wa shule yake wenye
vyeti vya ndoa waviwasilishe kwake.
>>>’Kweli
tumepewa agizo hilo leo manispaa ya Ilala na tumetakiwa kuwasilisha
vyeti hivyo kesho na tayari baadhi ya walimu wangu wamefanya hivyo leo
na kesho zoezi hilo linakamilika‘
Alipoulizwa
sababu ya kuwepo kwa zoezi hilo, mwalimu huyo alisema hajui lakini
anahisi lina lengo la kudhibiti taarifa za uongo za watumishi wakati wa
kuomba likizo.
Wakati walimu wa shule za Ilala
wakitakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ndoa, wilaya nyingine za Temeke,
Kinondoni, Ubungo na Kigamboni hawana taarifa hizo.
Mmoja wa walimu kutoka Manispaa ya Ilala
alisema kuwa uhakiki huo una lengo la kutaka kuchelewesha zaidi malipo
na stahiki za walimu za likizo ambazo hazijalipwa kwa miaka mingi.
No comments:
Post a Comment