Kijana
mkazi wa Unyakhae nje kidogo ya mji wa Singida, Said Mnyambi (26)
amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kunyofolewa
kipande cha ulimi wake na mke wa jirani yake aliyekuwa anamlazimisha
kufanya nae mapenzi.
Kwa mujibu
ya maelezo ya kijana huyo, tukio hilo limetokea siku ya Idd El Haji
Jumatatu wiki hii saa 3:30 usiiku.Alieleza kuwa siku ya tukio, mke wa
jirani yao mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake, alimwomba
amsindikize nyumbani kwa kuwa amelewa .
Alidai
walipofika njiani,mama huyo alimtaka wafanye naye mapenzi jambo ambalo
kijana huyo alimkatalia lakini alimwomba angalau waagane kwa kunyonyana
ulimi (denda) naye akamkubalia.
‘Nilimkubalia
kumpa denda na hapo ndipo alipoanza kufungua mkanda wa suruali yangu,
lakini nilipomkatalia kufungua mkanda wangu hapo ndipo alipong’ang’ania
ulimi wangu hadi akanyofoa kipande na yeye akakimbilia kwake’;- Said Mnyambi
Alipoulizwa
iwapo mama huyo ni mpenzi wake, kijana huyo alikataa kata kata na
kujitetea kuwa alimuomba amsindikize kwa vile tu anamfahamu na ni jirani
yake.
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dk Ramadhani Kabala
alithibisha kunyofolewa kwa kipande cha ulimi wa kijana huyo na kueleza
kuwa alifika hospitalini hapo kwa matibabu baada ya ulimi wake kupata
maambukizi na kuingia usaha hadi kushindwa kuongea.
Source Habari Leo
No comments:
Post a Comment