Tuesday, November 1, 2016

PICHA: WORLD VISION YAKABIDHI VIFAA VYA KUJIFUNGULIA KWA ZAHANATI TANO WILAYANI LONGIDO

Shirika la World Vision kupitia Mradi wake wa Maendeleo ya jamii Ketumbeine, umetoa msaada wa Vifaa vya Hosipitali vitakavyosaidia katika kurahisisha shughuli za Uzazi katika Zahanati tano zote zilizopo katika tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido Mkoani Arusha.
Akizungumza katika Makabidhiano ya vifaa hivyo, Mwezeshaji wa Mradi huo Ndugu Elisante William amesema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni ili kupunguza tatizo la wanawake wanaojifungulia Majumbani ambapo muda mwingine inapelekea vifo vya wanawake wengi wajawazito pamoja na watoto.
"Shirika letu la kijamii kupitia mradi wake wa maendeleo Ketumbeine AP, tunayo furaha kukabidhi  kwa jamii ya Ketumbeine vifaa  vya Hospitali vitakavyo kabidhiwa katika Zahanati tano ambazo ni Noondoto, Losirwa, Lang’atadapash, Ilerienito, na Gilai Merugoi ambapo ni imani yetu kuwa vifaa hivi vitasaidia  kwa asilimia kubwa kupunguza tatizo la vifo kwa wanawake wajawazito vinavyosababishwa na kujifungulia Majumbani kutokana na ukosefu wa vifaa stahili katika zahanati" Alisema Elisante.
"Kwa takwimu za haraka haraka inaonyesha kuwa katika jamii hii kati ya wanawake mia wanaojifungua ni wanawakewatano tu ndo wanajifungulia hosipitali na hii nikutokana na umbali wa vituo vya afya vyenye vifaa vya kujifungulia," Aliongeza.
Akipokea Msaada huo Kwaniaba ya Mkurugenzi wa wilaya ya Longido Ndg Atuganile amesema kuwa wanapongeza shirika la World Vision kwa kuona changamoto katika sekta ya Afya iliyopo wilayani 

Bw Elisante William wapili kutoka kulia ambaye nimwezeshaji wa Mradi wa Afya  akikabidhi seti ya vifaa vya kujifungulia(Delivery Kit) pamoja na Vitanda vya kujifungulia(Delivery Beds) kwa  Bibi Atuganile  Chisunga anayepokea kwaniaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido.
Bibi Atuganile akitoa neno la Shukrani baada yakupokea Msaada huo.
 

No comments:

Post a Comment