Afisa
Habari na Mawasiliano wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Chichi Banda
akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi ya sh Milioni 2 kwa Mwenyekiti
wa Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Majuto Omary kwa
ajili ya ziara ya mkoani Arusha kwa ajili ya kushiriki tamasha la
waandishi wa habari wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini
Afisa
Habari na Mawasiliano wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Chichi Banda
akikabidhi mfano wa hundi kwa Mwenyekiti wa Timu ya Waandishi wa Habari
za Michezo nchini, Majuto Omary kwa ajili ya ziara ya mkoani Arusha kwa
ajili ya kushiriki tamasha la waandishi wa habari wa mikoa ya Kanda ya
Kaskazini
Na Mwandishi wetu
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) imeendelea kuisadia timu ya Waandishi wa
habariza michezo nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidh Sh milioni 2 kwa
ajili ya kufanikisha safari yao ya kwenda mkoani Arusha kushiriki
katika tamasha la Waandishi.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Afisa Mawasiliano wa Benki ya Posta Tanzania
(TPB) Chichi Banda alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya shughuli za
Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini.
Chichi
alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaTaswa SC ambayo
inakwendakuteteaubingwa wake katika tamashahiloambaloufanyika kila
mwaka. Chichi alisema kuwa hii nimara ya tatu kwa TPB kuisaidiatimu
hiyo.
Awali
TPB ilikabidhi timu hiyo vifaa vya michezo napesa kwa ajili ya ziaraya
mkoani Arusha na kufanikiwa kufanya vyema katika ziara hiyo kwa kuutwaa
ubingwa ambao ina kwenda kuutetea mwaka huu.
“Waandishi
wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli,
wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa
faraja kubwa sana kwetu, ”alisema Chichi.
Mwenyekiti
waTaswa SC, MajutoOmaryaliishukuru TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na
kuahidi kutumia pesa hizo kwa ajili ya kufanikisha ziara yao katika
maadhimisho ya tamasha la waandishii wa Habari jijini Arusha.
“Tunajivunia
uwepo wa Benki ya Posta kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya
Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao
katika benki hii na vile vilekuomba wadau wengine kufuata mfano kwa
kuisaidiaTaswa SC ili iweze kufanikisha ziara zake,” alisema Majuto.
Majuto
alisema kuwa bado timu yao inahitaji msaada zaidi ili kufanikisha ziara
hiyo ambayo itawajumuisha wachezaji wa soka na netiboli. “Tunaishukuru
Benki ya Posta, pia tunawaomba wadau wengine nao waunge mkono, muda bado
upo,” alisema. (P.T)
No comments:
Post a Comment