Sunday, August 14, 2016

MGOSI ASTAAFU SOKA SASA KUWA MANAGER WA TIMU


 Mshambuliaji wa soka wa timu ya  Simba, Mussa Hassan Mgosi, akiwa na mwanawe, mara baada ya kucheza dakika tatu uwanjani kwenye pambano la soka la kirafiki baina ya timu yake na URA ya Uganda kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 14, 2016. , na kustaafu soka  Mgosi aliyechezea simba kwa misimu 10 amestaafu soka na sasa atakua meneja wa timu hiyo. Miongoni mwa watu waliohudhuria sherehe hiyo ya kustaafu kwake, ni pamoja na Familia yake, mkewe Jasmin na watoto wake watatu. Katika pambano hilo la kirafiki baina ya Simba na URA, matokeo yamekuwa sare ya kufungana magoli  1-1. (PICHA NA K-VIS B;LOG/KHALFAN SAID)
gosi
 Mgosi akikokota mpira mbele ya mchezaji wa URL kwenye pambano la soka la kirafiki kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 14, 2016

 Familia ya Mgosi ikiongozwa na mkewe Jasmina, (katikati) na watoto wake, Amina (kushoto) na Hassan wakipiga makofi baada ya Mgosi kustaafu soka kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam

 Mchezaji wa Kimataifa wa Simba, Laudit Mavugo, akiipasua ngome ya URL

 Ibrahim Ajib, akikokota mpira

No comments:

Post a Comment