Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa akifungua mkutano wa wanahisa wa benki hiyo katika Hoteli ya
Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akizungumza wakati wa mkutano wa
wanahisa uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti waBodi yaWakurugenzi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na baadhi ya
wanahisa wa benki hiyo kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa
hisa stahili za benki hiyo unaoanza Juni 26 hadi Julai 16. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na wanahisa wakimsikiliza Dk. Charles Kimei.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na wanahisa wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na mameneja wa matawi wakiwa katika mkutano huo.
Meza Kuu.
Dar es Salaam, Tanzania
BENKI
ya CRDB, imetangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa Hista
Stahili kwa wanahisa wake, unaofunguliwa Juni 26 na kuhitimishwa Julai
16, ili kuongeza mtaji wake wa uendeshaji.
Hisa
Stahili ni zile za ongezeko zinazotolewa au kuuzwa kwa wanahisa wa benki
hiyo kwa mfumo wa hisa moja mpya kwa kila hisa tano anazomiliki.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mauzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,
Dk. Charles Kimei, alisema kuwa baada ya maazimio ya wanahisa wake wote
katika Mkutano Mkuu uliopita.
“Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, imeidhinisha kuingiza sokoni hisa mpya
435,306,432 kwa ajili ya wanahisa wake ambapo kila hisa moja itauzwa kwa
shilingi 350, hivyo kusanyo tarajiwa la mtaji mpya litakuwa ni sh.
152,357,251,200,” alisema Dk. Kimei.
Alibainisha
kuwa fedha hizo zitakazopatikana baada ya mauzo ya hisa zitatumika kwa
mambo kadhaa, ikiwamo uboreshaji wa njia za kutolea huduma kwa wateja wa
benki hiyo.
“Mwanahisa
atakayekuwa na sifa za kupokea kupokea hisa hizi ni yule tu atakayekuwa
kwenye kumbukumbu za vitabu vya benki mpaka kufikia Alhamisi Juni 18
mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya mwisho ukusanyaji kumbukumbu hizo,”
alifafanua Dk. Kimei.
Aliongeza
kuwa CRDB inahitaji kuongeza mtaji wake ili kufikia malengo yake ya
kibiashara, ikiwamo upanuzi wa mtandao na ununuzi mitambo ya uendeshaji.
“CRDB
imeona hii ndio njia sahihi na bora zaidi, kwani licha ya kuongeza
mtaji, pia inatoa fursa kwa wanahisa wetu kuongeza hisa zao sambamba na
umiliki wao wa benki hii,” alibainisha Dk. Kimei.

No comments:
Post a Comment