Friday, January 9, 2015

Umeisikia hii ya tembo waliovamia kijiji na kunywa pombe? Isome hapa

Elephant
Tembo walivamia kijiji kimoja India wakiwa wanatafuta chakula, wakakuta kuna pombe ikiwa imewekwa na wanakijiji kwenye makopo, wakanywa na kulewa.
Mbaya zaidi baada ya kulewa walianza kufanya fujo, wakawa wanaangusha nguzo za umeme katika kijiji hicho na baadaye tembo  sita kati ya 40 walikufa baada ya kupigwa shoti na nyaya za umeme.
Hii sio mara ya kwanza kwa tembo kufanya tukio la namna hiyo, mwaka 2007 waliwahi kufa tembo wengine waliovamia vijiji, wakanywa pombe na kufanya vurugu ikiwemo kuvunja nyumba za watu na kukata nguzo za umeme.

No comments:

Post a Comment