Thursday, December 11, 2014

PALE PUNDA WANAPOTUMIKA KUFIKISHA UJUMBE WA KUCHOSHWA NA UONGOZI WA KUKANDAMIZWA


TZA-PUNDA WENYE GRAFITTI
Kenya ni moja ya nchi ambazo huwa zinakaa kwenye headlines ya kuwa na story kubwa Afrika Mashariki, ya leo inahusu punda waliobebeshwa ujumbe maalumu na kuachwa katikati ya jiji la Nairobi.
Desemba 11 katikati ya jiji la Nairobi katika moja ya barabara zenye shughuli nyingi ya Moi, lori moja lilisimama na kushusha punda wapatao 22 walio na maandishi yenye ujumbeTumechoka”.
Wanaharakati nchini Kenya wametajwa kuhusika na hii ambapo pia wamewahi kutumia njia mbalimbali ili kufikisha ujumbe wao ambapo moja ya waliyowahi kuifanya ni ile ya kuyabeba majeneza idadi sawa na Wabunge.
Taarifa zinasema kuwa huu mtindo wa kuwashirikisha wanyama kwenye maandamano ya kudai haki ilianzishwa na mwanaharakati ambaye pia ni mkurugenzi wa Pawa 254, Boniface Mwangi japo safari hii haijafahamika sababu ya kuwatumia wanyama hao kufikisha ujumbe huo.
Tumechoshwa na uongozi mbaya… ” alisikika mmoja ya wanaharakati huku akiwasukuma punda hao kutoka nje ya Lori.
Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.
TZA-WANANCHI WAKISTAAJABU PUNDA WENYE GRAFITTI
TZA-UJUMBE WA PUNDA
141211133827_donkeys_7 (1)

No comments:

Post a Comment