Monday, December 15, 2014

NEY WA MITEGO KUFANYA MAKAMUZI ARUSHA JUMAMOSI HII

Msanii wa muziki wa kizazi kipya  Ney wa Mitego anatarajiwa kulipamba Tamasha la amani linalotarajiwa kufanyika mapema jumamosi hii desemba 20 katika viwanja vya Sheik Amri Abeid lililoko mkoani Arusha.


Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa Tamasha hilo Bertha Ismail kupitia kampuni ya Bimo media alisema kuwa Msanii huyo anaetamba na wimbo wake wa “Nakula Ujana” anatarajiwa kutua mkoani Arusha siku ya Alhamisi ya desemba 18 na timu yake nzima ambapo atafanya matangazo katika sehemu mbalimbali za jiji la Arusha kuhamasisha watu kuhudhuria tamasha hilo.

“Mbali na wasanii wengine wa Arusha, Msanii mkubwa ambae anatarajiwa kulipamba tamasha hilo ni Ney wa Mitego ambae tunaamini kwa Arusha atavuta watu wengi kuhudhuria tamasha katika uwanja wa Sheik amri abeid kuja kusikiliza ujumbe wa Amani ambapo utatolewa na Mgeni Rasmi”alisema Bertha.

Alisema kuwa Tamasha hilo litakalohudhuriwa na viongozi mbali wa serikali, Tasisi pamoja vyama vya siasa, lengo kubwa ni kuwaunganisha vijana na kupata ujumbe wa amani hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwakani, ujumbe utakaotolewa na msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi.


“Tunapoelekea uchaguzi tunajua mara nyingi sisi vijana ndio tunaotumika zaidi, hivyo lengo kuu la Tamasha hili ni kuwaunganisha vijana katika umoja  ili wasigawanywe kwa misingi ya dini na siasa hali itakayojenga chuki na kufanyiana fujo, hivyo wasifanye hivyo bali kila mmoja atumikie chama chake au dini yake kwa amani bila vurugu”

Bertha alisema kuwa Tamasha hilo lililodhaminiwa na kiwanda cha soda cha pepsi, Kituo cha redio five na Sunrise Arusha, Mbali na Burudani ya Ney wa mitego pia kutakuwa na burudani zingine kama Ngoma za asili, sarakasi, maonyesho ya warembo wa mitindo pia vijana chipukizi wa Arusha wataimba nyimbo mbali mbali sambamba na Watangazaji wa redio za Arusha kukimbia riadha hivyo kutumia fursa hiyo kuwaalika wadhamini kutumia nafasi hiyo kutangaza bidhaa zao kwa kushiriki tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment