Thursday, July 10, 2014

Walichofanywa maafisa waliouza tiketi haramu za Kombe la dunia Brazil.

tickets
Polisi nchini Brazil wanasema kuwa watu 12 akiwemo mkurugenzi wa kampuni iliyopewa dhamana ya kuuza tiketi za Mechi za Kombe la dunia wamesimamishwa kazi.
Hatua ya kuwasimamisha kazi ni kutokana na kashfa ya kuuza kiharamu tiketi za kuangalia mechi za kombe la Dunia.
Ray Whelan, anayefanyia kazi kampuni hiyo inayoshirikiana na shirikisho la kandanda duniani FIFA, ametiwa mbaroni, na watu hao wengine katika mji mkuu Rio de Janeiro.
Viongozi wa mashtaka hivi sasa wataamua iwapo watu hao watafunguliwa mashitaka au la.

No comments:

Post a Comment