Baada
ya kuripotiwa kuwepo kwa mabadiliko ya noti ya sh. 500 ambayo itaacha
kutumika siku chache zijazo nchini Tanzania na mbadala wake kuwa sarafu
ya shilingi 500, Watanzania mbalimbali wamekuwa na wasiwasi na taarifa
hiyo pamoja pia na kuamini uchumi wa nchi unaanguka.
millardayo.com imepata nafasi ya
kuongea na mchumi wa benki kuu kwenye kurugenzi ya utafiti na sera za
uchumi Lusajo Mwankemwa ambae amejibu hizo headlines kwa kusema hiki
kifuatacho.
‘Kwa niaba ya benki kuu ya Tanzania
amewatoa hofu kuhusu haya mabadiliko na kusema haijaja kutokana na
ukuaji na ushukaji wa uchumi wa nchi ya Tanzania, yaani kuanza kutumika
kwa hii sarafu hakuhusiani na Tanzania kushuka kiuchumi’
‘Noti
ya 500 imeonekana inachakaa sana ndani ya miezi 6 kutokana na kuwa na
mzunguko mkubwa ikilinganishwa na noti nyingine na haipitii ule mfumo wa
kawaida wa kibenki kurudi benki kuu kwa ajili ya kuibadilisha,
tulitarajia Mwananchi anapokwenda bank kupeleka pesa zake basi na 500
iwe miongioni mwa hizo pesa ili tuzibadilishe kwa kutoa noti mpya ambazo
tunazo benki kuu lakini haijawa hivyo’
‘Tumegundua Mwananchi anaitumia ile
mia tano huku chini ambapo pesa anazopeleka benki ni shilingi elfu
mbili, elfu 5 na elfu 10 lakini 500 anabakiza kwenye droo kwa ajili ya
matumizi madogomadogo, matokeo yake inatumika huku chini kwenye mikono
ya watu na haipati kurudi kwenye mfumo wa kibenki kubadilishwa ndio
maana tumeona ni busara kuiondoa na kuleta sarafu’
‘Kiuchumi hili halina muingiliano wa
moja kwa moja, itambulike kwamba kinachofanywa ni kuondoa noti ya 500
yenye thamani ya 500 na kuleta sarafu yenye thamani ileile ya shilingi
500, kwahiyo thamani iko palepale’
No comments:
Post a Comment