Monday, June 16, 2014

Kutana na Ngamia mtabiri wa mechi za kombe la dunia na matokeo ya utabiri wake

Kwenye miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na matumizi ya wanyama na viumbe wengine kwenye kutabiri matokeo ya mechi za soka hasa kwenye michuano mikubwa kama kombe la dunia.

Mwaka 2010 wakati wa WOZA, nchini Ujerumani kulikuwa na Pweza ‘Octopus Paul’ ambaye alitabiri mechi zote na akapatia kila utabiri, mwaka huu amekuja Ngamia aitwaye Shakeeen kutoka Dubai ambaye nae alianza kutabiri tangu siku ya kwanza.
20140616-102950-37790371.jpg
Shakeen ambaye anamilikiwa na shabiki mmoja wa timu ya soka ya Al Wasry ya Dubai, alitabiri mechi zote za ufunguzi na akapatia, akatabiri ushindi wa Italy dhidi ya England akapatia, jana akaitabidi ushindi Ufaransa na Argentina akapatia tena.
Pia ameitabiria Ureno kushinda mechi ya leo dhidi ya Ujerumani.
20140616-103044-37844157.jpg
 

No comments:

Post a Comment