Friday, June 13, 2014

Familia za waliopotea kwenye ndege ya Malaysia wapozwa, waanza kulipwa fidia.

ndugu2
Familia za abiria waliopotea na ndege ya Malaysia wameanza kupokea malipo ya awali ya fidia ya dola elfu 50 kila mmoja.
Mpaka sasa, Familia sita kutoka Malaysia na moja ya China wamepokea fedha hizo na makampuni ya Bima yanadai kiasi cha fedha kwa familia 40 zaidi.
ndugu
Ndugu wa abiria wote 239 waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanaweza kudai fedha taslimu takribani dola laki moja na elfu 75 kila mmoja.
Ndege ya Malaysia yenye namba MH370 ilipotea Machi 8 mwaka huu wakati ikisafiri kutoka Kuala Lumpur hadi Beijing ambapo hadi sasa haijapatikana.

No comments:

Post a Comment