Kikosi cha zimamoto kikiizima helkopta hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania iliyokuwa imewabeba viongozi wa serikali.
MAKAMU wa Rais Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Said Mecky Sadick, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova na mpiga picha wa TBC, George Kasembe wamenusurika kifo
baada ya helkopta waliyokuwa wanasafiria kupata ajali Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere. Viongozi
hao walikuwa katika helkopta ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa
ziara ya kukagua athari za mafuriko jijini Dar es Salaam.
Baada ya ajali, viongozi hao wamepatiwa matibabu katika majeraha waliyoyapata na wameendelea na ziara yao!Credit GPL
No comments:
Post a Comment