Thursday, January 30, 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA MBOWE AMTAMBULISHA AFANDE SELE KWENYE OPERESHENI YA M4C MJINI MOROGORO

Halima Mdee: Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.

Mbowe na Afande Sele: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro jana.

Afande Sele: Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro jana, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoj Daima, ambao pia ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
Mbowe, Halima wakiondoka Ifakara: Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara jana.
Mkutano Ifakara: Maelefu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana.
Mabango Ifakara: Baadhi ya wananchi mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.

Wananchi Ifakara: Sehemu ya maedlfu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakitawanyika baada ya mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
(Picha na JF

No comments:

Post a Comment