Thursday, January 30, 2014

UNAAMBIWA MASTAA WENGI WA BONGO HAWAJIELEWI KABISA, WANAISHI KWA MAJINA TU MJINI LKN HAKUNA CHOCHOTE,

MAKALA: Gladness Mallya
NITAELEWEKA tu! Sina ubishi kwamba kwa sasa Bongo, fani ya sanaa ya uigizaji ndiyo imeshika kasi kukubalika katika jamii (anayebisha anyooshe mkono, najua hakuna).

Elizabeth Michael 'Lulu'.
Siku hizi ukikatisha kwenye mitaa mbalimbali nchini Tanzania, hasa uswahilini, utagundua wengi wanaangalia ‘filamu za akina Kanumba’ kama vile Uncle JJ, Ndoa Yangu, Mr. Ben, World of Benefit na nyingine nyingi.

Haya ni maendeleo kwa wasanii wetu ambao zamani walikuwa wakihaha kutoka lakini walishindwa kutokana na soko la filamu Bongo kushikwa na ‘muvi za akina Rambo’ na baadaye akina Noa Ramsey.

ANGALIZO LANGU
Pamoja na yote hayo, kuna angalizo langu. Ili sanaa hiyo izidi kukua nchini ni lazima kuwe na ushirikiano mkubwa kati ya wasanii wenyewe (waigizaji) na vyombo vya habari.

Aunt Ezekiel.
Vyombo vya habari ndivyo vinavyotangaza kazi zao mpaka zikajulikana na akina mama Nyakomba kule kijijini Songea (nyumbi hii, bomba hii). 

Lakini kumekuwa na ugumu wa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya waigizaji, hasa wale ambao wanajiita (hawaitwi) wanajiita masupastaa au mastaa wa Bongo (Bongo Movies).  
 

Hawa jamaa baada ya kuamini wamekuwa na majina makubwa kupitia filamu (ni vyombo vya habari vilivyowafanya wawe na majina makubwa) wamekuwa na dharau, wamekuwa bize, wamekuwa hawana nafasi, simu wamekuwa wakiziweka mbali na wao walipo au hazina chaji tangu jana usiku (si unajua umeme wa Tanesco?).


Jack Wolper.
MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, hao ‘mastaa’ wapo hata wale waliokwishaonekana kwenye filamu tatu tu tena si ‘mastering’, waliigiza kwenye udereva, kufungua mageti, wakaribisha wageni maofisini au wasaidizi wa kazi za ndani ‘mahausigeli’.


NINAVYOJUA MIMI


Kwa mujibu wa ufahamu wangu mdogo ni kwamba, katika kila tasnia duniani kuna masupastaa na mastaa. Pia wapo wahusika wa fani husika. Kama filamu tunasema waigizaji.
Sasa hawa wa Bongo ambao nao pia wamejiweka kwenye kundi la masupastaa na mastaa wananitatiza kila kukicha, kwamba ni wagumu kupatikana, iwe laivu au kwa simu kwa sababu wao ni maarufu katika fani.

Jacob Steven 'JB'.
MASUPASTAA
Kufuatia lawama zangu hizi kwa wasanii wa fillamu Bongo, kama mtu ataniuliza ninavyojua mimi nani supastaa, staa na mwigizaji orodha yao ninayo na niko tayari kuiweka wazi.


Siwezi kusema Ray, JB, Aunt Ezekiel, Nora, Wolper, Johari, Natasha, Monalisa, Dk. Cheni, Riyama Ali, Lulu, Mzee Majuto, Mzee Small siyo mastaa wa filamu Bongo.


Wamecheza filamu nyingi, wamejenga majina makubwa kupitia sanaa hiyo. Japokuwa miongoni mwao wapo ambao ni wababaishaji kwenye kupokea simu na kujifanya ‘aghali’ kupatikana.
 

Lakini pia kuna kundi la mastaa wa filamu za Bongo; hawa ni akina Baba Haji, Kuambiana, Maya, Jini Kabula, Wastara, Mr. Chuz, Frank Mwikonge, Mzee Chilo, Mzee Magali, Cloud, Penina, Richie, Bi. Chau na Thea.
 

Wengine ambao kwangu ni mastaa ni, Jack wa Chuz, Cathy, Lucy Komba, Big, Chekibudi, Baba Haji, Kelvin, Odama, Rose Ndauka, William Mtitu, Tino, Flora Mvungi, Nisha, Shilole, Mainda, Shamsa Ford, Snura, Mlela, Shumileta, Hemed, Yusuf Mlela, Dude na Maya.
 

Mbali na makundi hayo, kuna ambao wamepitiliza usupastaa na sasa wameingia kwenye kundi la wakongwe wa sanaa. Hawa ni kama akina Natasha, Mzee Small, Mzee Majuto, Bi. Hindu, Bi. Mwenda, Bi. Chau, Kemmy na Muhogo Mchungu.



Mzee Majuto.
Lakini napata tabu kusema, Batuli, Zamda, Tiko, Slim, Skaina, Rachel Haule, Chikoka, Kupa, Mafufu, Badra na wengine wengi ambao kwenye fani hawana hata mwaka mmoja ni mastaa.
Kwa nchi za wenzetu ‘majuu’, vyombo vya habari havitambulishi kila mwigizaji kama staa, ila wanakuwa mastaa katika filamu walizocheza tu, hususan kama amecheza filamu mbili au tatu.

Mfano; wakitaka kumtambulisha Rachel Haule watasema: “Staa wa filamu ya…..(wataitaja jina), Rachel Haule amepata mchumba (mfano lakini).

Majuu staa, kama wa filamu ni yule aliyekwishacheza muvi zaidi ya 10 akiwa ni stering na zikatikisa. Kibongobongo, hata akicheza filamu moja halafu akavuma sana, tena wengine huvuma kwa mambo nje ya filamu, ni staa.
Makala haya ni mtazamo wangu.

Taarifa ya kifo na mazishi ya mchekeshaji mzee Dude.




Mzee Dude msanii wa tasnia ya maigizo toka kundi la Futuhi linalorusha kazi zake kupitia Star TV amefariki dunia jana saa 11 jioni akipatiwa
matibabu katika Hospitali ya  Bugando ya jijini Mwanza.
Marehemu mzee Dude alilazwa mara baada ya kuzidiwa ugonjwa wake wa muda mrefu aliokuwa nao wa figo kushindwa kufanya kazi.
Mzee Dude alikuwa mchekeshaji na atazikwa leo jijini Mwanza majira ya alasiri.
- See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2014/01/taarifa-ya-kifo-na-mazishi-ya.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FhgdRs+%28Onelove+Tz%29#sthash.tFXwXtlx.dpuf

No comments:

Post a Comment