Sunday, January 26, 2014

HABARI+PICHA..JUAN MATA RASMI NDANI YA O.T MAN UTD....JIONEE HAPA.....

Manchester United imekamilisha rasmi usajili wa kiungo Juan Mata kutoka Chelsea kwa ada ya usajili ya £37.1 million, ambayo ni rekodi mpya katika usajili wa United, klabu hiyo imethibitisha.

Mata, 25, ameshaichezea mara 32 timu ya taifa ya Spain na amecheza mechi  Chelsea, akifunga mabao 32 tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Valencia mwaka 2011. 

Juan Mata alinukuliwa na mtandao wa Man U akisema: “Nina furaha sana kujiunga na United. Nilikuwa ni muda mzuri sana Chelsea lakini muda umefikia kwa changamoto mpya. United ni sehemu sahihi kwangu na nina shauku kubwa ya mmoja ya waliopo katika historia mpya ya klabu hii.
“Chelsea ni timu kubwa na nina marafiki wengi pale lakini huwezi kukataa nafasi ya kujiunga na Manchester United.” – Mata

No comments:

Post a Comment