Saturday, October 19, 2013

YOUNG 'D' ASEMA UKWELI KUHUSU YEYE KULA UNGA

 
Msanii Young Dee amekanusha uvumi ulioenea mitaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa pamoja na story hizo kuwa kubwa lakini hali hiyo haijamuathiri sana kwasababu hazina ukweli wowote.

“Ni story ambazo zimekuwa kubwa sana lakini hazijaniathiri sana kwasababu sio ukweli, lakini zimenifanya nimezidi kuwa makini sana kuwa muoga pia na vitu vingi sana kuangalia watu wanaonizunguka, mazingira na vitu kama hivyo”.
Alisema Young Dar es salaam kupitia E-News ya EATV jana .
Dee amesema kuwa anafahamu fika kuwa utumiaji wa ‘unga’ unaweza kuathiri kazi yake ya muziki kutokana na mifano hai ambayo imeshaonekana kwa wasanii wengine,

“The more the story zinakuwa kubwa zinapoteza maana nzima ya kitu nachohangaikia kila siku ambayo ni muziki, so naonekana muziki nafanya nakula unga na mifano ipo watu ambao wameingia kitika hayo mambo”.

Young Dee alimaliza kwa kusema kama kweli maneno yanayosemwa mtaani yana ukweli basi watu watagundua haraka, “mi ambacho naweza kusema unga hauna siri haufichiki so kama mi nakula unga people they can easily notice haraka sana”.

No comments:

Post a Comment