Saturday, October 19, 2013

KUTANA NA MWANAMUZIKI MZURI WA KIAFRIKA AMBAYE AWALI ALIKUWA MWANAUME

Titica

Mwanamke huyu kwa jina akijulikana kama Titica, amekuwa ni gumzo kubwa nchini Angola.
Siku chache zilizopita UNAIDS ilimpa heshima mwanamke huyu aliyejibadili jinsia kuwa Balozi wake.

Alizaliwa Luanda kama Teca Miguel Garcia, akiwa muimbaji na mchezaji, Titica alibadili maumbile yake miaka minne iliyopita mara
baaada kufanya upasuaji wa maziwa nchini Brazil.

Sasa, akiwa na miaka 26, Titica amekuwa

kioo cha Angola kwa aina ya muziki anaoufanya
wenye mchanganyiko wa miondoko ya rap na
techno unaojulikana kama “kuduro”.

Akiongea na BBC mwaka jana, akiwa kwenye kwenye utengenezwaji wa video ya wimbo wake unaotamba sasa uitwao Olha o Boneco, wimbo
ambao amemshirikisha muimbaji mashuhuri wa muziki aina ya kizomba aitwaye Ary, Titica alisema amefanikiwa kukabiliana na vikwazo vyake.

“Shukrani kwa Mungu, nina furaha sana, imechukua muda kufika hapa na imehusisha mambo mengi ya kujitolea ila asante Mungu,
kila kitu kinakwenda sawa kwangu.

Nilikuwa nikipigwa mawe, nimekuwa nikipigwa na kumekuwa na vikwazo vingi vya kisheria dhidi
yangu, watu wengi walionyesha hilo. Kuna miiko mingi sana,”.

Licha ya miiko hiyo, bado Titica anaonekana kuwa hana upungufu wa mashabiki huku wengi wakiwa wanavutiwa zaidi na muziki wake kuliko
jinsia yake.


No comments:

Post a Comment