Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa mbaroni na polisi
Kijana ambae amekuwa akiwaliza
watumishi mbalimbali wa umma na watu binafsi kwa kutumia jina la
waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge kijana
Jonathan Wiliam Lukuvi( si jina lake halisi)amekamatwa katika hafla ya
kanisa la Overcomers FM akitaka kumtapeli waziri mkuu wa zamani
Edward Lowassa kupitia harambee hiyo.
Kijana huyo aliingia katika ukumbi
wa St. Dominic juzi katika harambee ambayo mgeni rasmi alikuwa ni
Lowassa na kupita mbele na kutumia kipaza sauti kuzungumza kuwa
anaitwa Jonathan Wiliam Lukuvi na ni mtoto wa waziri wa nchi ofisi
ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na kuwa amekuwa akimpigia
simu mara kwa mara Lowassa na hata katika mkutano wake wa Jangwani
jijini Dar es Salaam alipata kuzungumza na Lowassa na hivyo kuomba
kutekelezewa ombi lake la msaada ambao hakuutaja.
Kutokana na utambulisho huo baadhi
ya watu waliopata kutapeliwa na kijana huyo akiwemo mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa waliweza kuguna hali iliyopelekea
askari polisi kufunguka na kumtia mbaroni kijana huyo ambae alikuwa
akiweka mtego wa kumtapeli Lowassa na viongozi wengine katika hafla
hiyo .
Hata hivyo baada ya polisi kumtia
nguvuni kijana huyo baadhi ya watu waliotapeliwa waliweza
kumtambua huku familia ya Lukuvi iliyokuwemo katika ukumbi huo
ikimkana katu katu kuwa hana hata chembe ya familia na watu
hawamtambui .
Kada wa CCM maarufu mkoani Iringa
Godfrey Malenga Lukuvi alisema kuwa kijana huyo amekuwa akitumia
jina la waziri Lukuvi kuliza watu na kuwa wengi wamekuwa
wakilalamika kuhusu utapeli unaofanywa na kijana huyo na kuwa tayari
alipata kukamatwa na polisi ila alitolewa .
Kwa upande wake katibu wa mbunge
jimbo la Isimani ambae pia ni familia ya Lukuvi Bw Thom Malenga
Lukuvi alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa
watu mbali mbali ambao wamelizwa na kijana huyo na kuwa siku zote
alikuwa akiweka mtego ili kumnasa kijana huyo tapeli japo hakufanikiwa
kumpata.
Thom ambae yupo nje ya mkoa wa
Iringa kwa shughuli za kifamilia alisema kuwa alitamani sana kama
angebahatika kumshuhudia kwa macho kijana huyo tapeli ila kwa kuwa
yupo nje ya mkoa atajitahidi kurudi mapema mjini Iringa ili kumwona
tapeli huyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo alimweleza mwandishi
wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa pia kijana huyo alipata
kufika ofisini kwake kwa ajili ya kumtapeli na baada ya kumshtukia
alimtafuta waziri Lukuvi kwa simu na kuelezwa kuwa kijana huyo ni
tapeli mkubwa .
Hata hivyo mwanahabari Gerald
Malekela wa radio Nuru Fm alisema kuwa kijana huyo alipata kufika
studio za radio hiyo kwa ajili ya kutapeli uongozi kwa kutumia
jina hilo na kufika studi za radio hiyo huku akiwa na barua
inayosifia watangazaji na kuomba kusaidiwa zaidi kama mmoja kati ya
wasikilizaji .
Mtandao huu ulipata nafasi ya
kumtafuta kwa njia ya simu waziri Lukuvi ambae mbali ya kumkana
kuwa hamtambui bado alisema kuwa amepata kuwaliza watu mbali mbali
kwa kutumia jina lake.
Lukuvi alisema kuwa tayari amepata
kupokea malalamiko kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na
kumwagiza kumtakata na kutaka sheria ichukue mkondo wake.
"Mimi huyu kijana simtambui na
wala si ndugu yangu ila amekuwa akitumia jina langu kutapeli watu na
tayari alikamatwa na polisi kwa utapeli huo"
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk
Christina Ishengoma aliwaonya watu wanaoendelea kutapeli wengine
kwa kutumia majina ya viongozi ama namna nyingine yeyote kuacha mara
moja na kuwa akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa hatakubali kuona matapeli hao wakiendelea kulizwa watu kwa njia
ya udanganyifu .
Hata hivyo aliwataka wananchi
kujiepusha na wimbo hilo la utapeli kwa kuwaripoti polisi watu
wanaowashukia kuwa ni matapeli.
No comments:
Post a Comment