Wanafunzi wagomea masomo na kudhamiria kuandamana kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kisu usiku wa jana, saa nne usiku wakati akitokea chuo kujisomea. Katika picha ni matukio yanayoendelea sasa chuoni hapo, wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha bwana Godbless Lema..
Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kime0.lazimika kutumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi hewani kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wametanda chuoni hapo na kugoma kumsikiliza mkuu wa mkoa, kwa madai kwamba ana dharau. Mabomu na risasi zilirindima eneo hilo huku wanafunzi wakikimbia hovyo huku na kule kwa hofu na woga
MKUU WA MKOA AGOMA KUONGEA NA WANAFUNZI KWA MADAI HAWEZI KUONGEA BILA KIPAZA SAUTI!!!
"Mkuu wa mkoa mwenyewe anaitwa hapa kwenye tukio anakuja kama anakuja kwenye send-off wakati kaitiwa msiba hapa" Ni maneno ya mbunge wa jimbo la Arusha bwana Godbless Lema.. pia Lema amesikika akisema "Mkuu huyo wa mkoa amekuja hapa si kwa ridhaa yake, bali ni cheo tu kimemleta hapa" Wanafunzi wa chuo hicho kwa sasa hawataki kusikia lolote ni maandamano tu wanatka..
No comments:
Post a Comment