MREMBO mmoja, Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar amebambwa akidaiwa kuiba fedha kwa njia za miujiza eneo la
Bunju Mwanjenje kwenye duka la Wapemba.
Imeelezwa
kuwa katika tukio hilo, Rukia alichukua fedha kimiujiza dukani na
kutokomea, hali iliyosababisha wenye duka kutangaza dau la shilingi
500,000 kwa atakayewezesha kukamatwa kwake.
Arobaini zake zilipowadia, Rukia alikamatwa akiwa mafichoni, Boko Mtambani na kushushiwa kichapo na wananchi wenye hasira
wakimtaka amtaje aliyemtuma.
Baada ya kupokea kichapo, mrembo huyo aliwataja baadhi ya watu akiwemo mganga mmoja anayetokea Sumbawanga (jina tunalo)
na kudai kuwa ndiye aliyekuwa akimpa dawa (chuma ulete).
“Dawa hiyo huwa naiweka kwenye pesa zangu nyumbani ili ziongezeke na nyingine huwa natembea nayo kwa ajili ya kujipatia
pesa,” alisema mrembo huyo.
Mrembo huyo alikiri kufanikiwa kuiba mamilioni ya shilingi kwa kutumia dawa hiyo na kuomba asamehewe. Rukia aliokolewa na
ndugu zake pamoja na wasamaria wema waliompeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo alikofunguliwa mashtaka ya wizi.
Tukio hilo ni la pili kwa Rukia kwani mara ya kwanza alikamatwa Tabata jijini Dar es Salaam miezi michache iliyopita kwa tuhuma
kama hizo lakini akaachiliwa baada ya kuomba msamaha.
chanzo:.globalpublisher
No comments:
Post a Comment