Tuesday, March 12, 2013

WAMILIKI NA MADEREVA WA MAGARI KUANZIA TANI MOJA MPAKA TANO WASHANGILIA KUFUTWA KWA SHERIA NDOGO YA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YA KUWATAKA WALIPE USHURU WA SH 58,000 KWA MWAKA

Meya wa Jiji la Mbeya Ndugu  Attanus Kapunga akiwaomba watulie ili awasikilize shida yao wamiliki na madereva wa magari ya biashara kuanzia tani moja
Makamu mwenyekiti wa chama cha wamiliki na madereva waendesha maroli jijini mbeya Gorden Mwamakula akieleze wanavyonyanyaswa na wakala aliyeteuliwa na jiji la mbeya kukusanya usajiri wa magari yao huku akiwatoza kiwango kikubwa na kuwalipisha faini zisizoeleweka

Paulo Mwasilelwa Dereva wa Pick up ambaye pia ni katibu
 wa Chama cha waendesha maroli Jiji la Mbeya amesema
 wanapingana na ushuru huo ambao unatozwa unawaumiza kwa sababu hulazimika kulipia gharama za usajili wa gari linaponunuliwa, bima ya gari,Tra, maegesho na zimamoto ambavyo lazima vilipiwe.
Wamiliki na madereva wao wakiwa makini kumsikiliza meya wa jiji la mbeya
Emmanuel Mbuza  mmilikiwa Mbuzax Auction Mart & Court Brockers akiingia ukumbini hapo huku madereva na wamiliki wa maroli wakimtolea macho
Moja ya wanasheria wa jiji la Mbeya Kaijage akielezea sheria inayotumika kukusanya ushuru huo wa maroli yanayofanya biashara katika jiji la Mbeya
Jamani kwakweli kiwango cha shilingi 58,000/ kwa mwaka ni kikubwa sana kwani kila siku tunalipa shi 1000 kwa maegesho ya magari yetu pili huyu wakala mliyempa kazi hii hatuelewi ni kigezo gani kilitumika kumpatia kazi hiyo kwani ni mnyanyasaji sana moja ya madereva akitoa malalamiko yake kwa meya
Mheshimiwa meya siku ytulipokuja ofisini kwako kukueleza juu ya huyu wakala wenu ukasema humtambui sasa leo nashangaa unasema unamtambua sasa tukueleweje hapo mweshimiwa meya unatuchanganya
Kwa ujumla huyu wakala hatumwelewi tunamlipa hiyo kodi risiti anatupatia za malipo ya Taxi 
Emmanuel Mbuza akinyoosha mkono ili apatenae kuzungumza kidogo hapo ndipo palikuwa pangumu kelele zilitawala ukumbi mzima kutaka akae la sivyo hali ya hewa humo ukumbini itachafuka

Naibu meya Fungo akijaribu kuwatuliza wamiliki hao wasiendelee na kelele jamani tumewaelewa Mbuza tunaomba ukae ili kikao kiendelee 
Ndugu zangu tumegundua kweli kwenye sheria hiyo kunamapungufu mengi ya kukusanyaji wa ushuru huo hivyo basi zoezi hili nalisimamisha mpaka tukakae na wenzangu ili tuiangalie upya sheria hiyo pia wakala huyu hata takiwa tena kukusanya ushuru huo kuanzia leo hapo ukumbi ulilipuka kwa vifijo na fulaha baada ya mweshimiwa meya kutamka tamko hilo
Jamaa wakiondoka kwa furaha kufuatia ushindi wa matatizo waliotoa kwa meya wa jiji la Mbeya

Emmanuel Mbuza amesema kutokana na kuvunjwa na kufutwa kwa sheria hiyo kutampunguzia yeye kufanya kazi katika mazingira magumu yanayosababisha kuwa na ugomvi na wananchi wanaotakiwa kulipia ushuru huo.

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya limelazimika kuifuta Sheria ndogo ya Halmashauri hiyo namba 376 (4)na (1) ya Mwaka 2011 iliyokuwa inataka kusajili magali ya kukodi, teksi,Bajaji na Pikipiki kwa kulipia ushuru Shilingi 58,000/=kwa Mwaka.

Sheria hiyo imefutwa  baada ya kutokea ugomvi mkubwa baina ya wamiliki na madereva wa magari kuanzia tani moja hadi tano nne na wakala aliyepewa zabuni ya kukusanya ushuru huo.

Ushuru unaolalamikiwa na wamiliki hao wa magari ni ule unaokusanywa na Halmashauri hiyo kupitia kwa wakala aliyejulikana kwa jina la Mbuzax Auction Mart & Court Brockers inayomilikiwa na Emmanuel Mbuza.

Wananchi hao walitoa malalamiko hayo kwenye mkutano wapamoja kati ya wamiliki wa magari, madereva na viongozi wa Halmashauri ya Jiji chini ya Meya uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri uliopo Sokomatola Jijini hapa.

Wakizungumza kwenye mkutano huo Madereva hao wamesema utaratibu wa ushuru huo unawaumiza sana kutokana na kuwa na gharama kubwa kama ushuru wa usajili kwa mwaka Shilingi 58,000/= pamoja na ushuru wa kuegesha magari kila siku shilingi 1000/=.

Paulo Mwasilelwa Dereva wa Pick up ambaye pia ni katibu wa Chama cha waendesha maroli Jiji la Mbeya amesema wanapingana na ushuru huo ambao unatozwa unawaumiza kwa sababu hulazimika kulipia gharama za usajili wa gari linaponunuliwa, bima ya gari,Tra, maegesho na zimamoto ambavyo lazima vilipiwe.

Amesema Kodi ya Maegesho ni zaidi ya Shilingi 360000 kwa mwaka hivyo ukiongeza na ushuru wa usajili gari haliingizi fedha yoyote badala yake linadumaza uchumi wa mwananchi wa kawaida ambapo aliongeza kuwa biashara ya magari hiyo haina uhakika kutokana nakutokuwa na wateja wanaoeleweka badala yake wanasuburi kukodishwa.

Wameongeza kuwa utaratibu unaofanywa na wakala huyo ni mbovu ambao walidai kuwa wakala huyo hutumia nguvu nyingi hali inayosababisha kuhatarisha maisha yao kutokana na watumishi wa wakala huyo kutumia mapanga kuwatishia maderev pamoja na kuwajeruhi.



Akijibu tuhuma hizo Meya wa Jiji la Mbeya Ndugu  Attanus Kapunga aliyekuwa amefuatana na Kamati ya Fedha ya baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo alisema kutokana na sheria iliyokuwa imepitishwa na madiwani hao kutotolewa elimu kwa wananchi wanaotakiwa kulipa kodi inamakosa.

Kapunga amesema kama sheria haileti amani baina ya wananchi inatakiwa iangaliwe upya hivyo wakala anatakiwa kusimama mara moja ili Sheria hiyo iangaliwe upya kwa maslahi ya maendeleo ya Jiji hilo.

Amesema kitendo cha wakala huyo kukusanya ushuru kinyume na maeneo aliyoaambiwa ni kosa kubwa ikiwa ni pamoja na kutumia ubavu kudai kodi ambayo Halmashauri haijamtuma ni kinyume na taratibu alizopangiwa.



Ameongeza kuwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kwenye sheria hiyo lazima wakala asimame asubiri vikao vikae upya na kuitazama upya ili isiwagombanishe na wananchi hali itakayosababisha uvunjifu wa amani.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbuzax Emmanuel Mbuza ambaye awali hakupewa nafasi ya kujitetea kutokana na madereva kumzomea pindi aliponyoosha mkono akitaka kujitetea hadi mkutano unafungwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa anaishukuru Halmashauri hiyo kwa kugundua mapungufu ya sheria zao.

Mbuza amesema kutokana na kuvunjwa na kufutwa kwa sheria hiyo kutampunguzia yeye kufanya kazi katika mazingira magumu yanayosababisha kuwa na ugomvi na wananchi wanaotakiwa kulipia ushuru huo.

Amesema kilichofanyika ni Hlmashauri ya Jiji kugundua kuwa sheria iliyokuwa ikitumika ilikuwa na mapungufu ambayo wakala asingeweza kuyajibu badala yake walipa kodi walikuwa wakitoa lawama ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake.

No comments:

Post a Comment