Monday, March 11, 2013

MWANAFUNZI AANGUKIA KWENYE DIMBWI LA MAJI YA MVUA NA KUFARIKI BAADA YA KUSHTULIWA NA HONI YA GARI

Wananchi pichani wanaonekana wakiwa na huzuni wakati wa zoezi la kuokoa mwili wa marehemu aliyefariki kutokana na kuingia katika eneo la kijitoupele akienda skuli asubuhi leo wakati mvua ikinyesha na kusababisha ajali hiyo.

Inataarifiwa kuwa watoto hao walikuwa wawili wakipita eneo hilo  na kushitushwa na honi ya gari ya daladala iliokuwa ikiwapita, ndipo ikabidi kusogea pembeni. Watoto wale wawili wakateleza katika  eneo hilo. Mmoja wao alijitahidi kutoka na kutaka kumuokoa mwezake lakini akashindwa kutokana na nguvu ya maji yaliokuwa yakipita katika mtaro huo unaokatiza barabara.

Jitihada za wananchi zilishindikana kuuopoa mwili huo uliokuwa umeganda katika mtaro huo na kikosi cha zimamoto wakachukua jitihada za kuchimba sehemu ya pili ya barabara hiyo na kuupata.

---
Picha zote, maelezo na taarifa shukrani: Othman Mapara wa ZanziNews blog
Picture
Wananchi wakiangalia sehemu uliotolewa mwili wa Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza wa skuli ya Kijitoupele , baada ya kuteleza na kuingia katika mtaro wa maji na huku mvua ikinyesha na kusababisha kuchukuliwa na maji na kuvutwa katika mtaro huo na kusababisha kifo chake, wakati akienda skuli asubuhi leo.na Picha ya chini ni eneo aliloteleza na kuingia katika mtaro huo katika eneo hilo wananchi wakiangalia baada ya kutolewa.
Picture
Gari la Wagongwa la Kikosi cha Uokozi Zanzibar likiondoka sehemu ya tukio baada ya kufanikiwa kuupata mwili wa mwanafunzi wa darasa la kwanza wa skuli ya Kijitoupele, baada ya kuteleza na kuingia katika mtaro huo ulioko katika barabara ya kwenda fuoni eneo la Kijitoupele Zanzibar.

No comments:

Post a Comment