Tuesday, March 12, 2013

Wanakijiji walilia Kadi na Bendera za Chadema


Na Bryceson Mathias, Kwa-Mayambi, Mvomero

WANANCHI wa Mvomero Kata za Mtibwa, Sungaji, Kanga na Diongoya, wamewalilia viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, wakiwaomba kuwapatia Kadi na Bendera hizo wapeperushe na kuwa Wanachama Halali.

Waliyasema hayo kwa viongozi wa chama hicho mwishoni mwa wiki katika Mkutano uliofanyika Kwa-Mayambi katika Kijiji cha Maarufu cha Kilimanjaro Mji Mdogo wa Madizini Mvomero, ambapo Madiwani wa Kata ya Mtibwa Lukas Mwakambaya na Juliana Petro walihutubia.

Wakimuanika Mkurugenzi Halmashauri ya Mvomero jinsi alivyofuja fedha za miradi ya maendeleo  Sh. Mil. 585/- Mwakambaya alisema, Huu si wakati wa usingizi ila ni muda wa kujiunga naChadema ili kuikomboa nchi ambayo wao wamefanywa kuwa watumwa. 

“Madiwani wa Chadema tuko watatu tu Halmashauri ya Mvomero lakini Mkurugrnzi Salar Linuma anakiona kiti chake cha Moto, maana tunafukua Uchafu, Ufisadi na Umangimeza wa Kodi yenu hadi nyuma ya Pazia ili muishi maisha Bora”.alisema Mwakambaya.

Alisema Kilio chao cha kutaka Kadi za Chadema na Bendera ili wanachama Halali na kupeperusha bendera hizo ili wawafahamu kuwa si Magamba tena ila watu wa Magwanda ya ukombozi, wamelisikia wataliwasilisha na anaamini Viongozi wake Kitaifa watalitekeleza haraka.

Kwa Upande wake Diwani wa Viti Maalum Juliana Petrol alisema, “Ni aibu kwa Mwanamke kula Chakula jikoni na kuwanyima watoto haii inayodhihirisha kuwa ni Mchoyo, hivyo alisema amesikitishwa kuona mwanamke mwenzao amefuja Mil. 585/- kwa miezi minane ni aibu kwao.

Aidha wananchi walio wengi walijiunga na Chama hicho, wakiusihi uongozi wa Kitaifa mbali ya kuwapatia Kadi na Bendera, uwatembele kila wakati na uwasaidie kuwatetea dhidi ya Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa kutokana na kuwasababishia Umaskini wa kutupwa.

No comments:

Post a Comment