Thursday, March 7, 2013

TCD YAWEKA WAZI MAAZIMIO YA KIKAO CHAKE

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia (TCD), Mh, James Mbatia akizungumza na waandishi wa Habari, (hawapo pichani)  juu ya maazimio ya kikao Maalum cha Viongozi wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge (TCD)  uliofanyika tarehe 06/03/2013.
 Baadhi ya maazimio ya kikao hicho ni kwamba Vyama viwe na umoja wa kitaifa katika mambo muhimu ya kitaifa kwa masilahi ya pamoja ya Taifa na kuondokana na ushabiki wa Itikadi za vyama katika bunge, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Spika kuwa na utaratibu wa mara kwa mara kushauriana na vyama vya siasa ili kuboresha ufanisi katika pande zote kwa Maslahi ya Taifa.

Kikao hicho pia kilipokea taarifa za tukio la kiharamia la kuvamiwa kwa Ndugu Absalomon Kibanda Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri na kulaani vikali tukio hilo.
Baadhi ya waandishi waliohudhuria katika kikao hicho

No comments:

Post a Comment