Thursday, March 7, 2013

BI AISHA SURURU AWAFARIJI WAKAZI WA MAJOHE WALIOPATWA NA KIMBUNGA

Mwanaharakati kutoka katika Shirika lisilo la kiserikali la Aisha Sururu Foundation na Diwani viti maalum katika Manispaa ya ilala Mh, Aisha Sururu akiangalia baadhi ya vitabu vya wanafunzi vilivyoharibiwa na Kimbunga kilicho ambatana na Mvua kubwa maeneo ya Majohe jijini Dar es Salaam wakati alipofanya Ziara maeneo hayo.
 Katika Ziara hiyo Bi, Aisha Sururu alibaini kuharibika kwa Nyumba 176 zilizoezuliwa Mapaa pamoja na uharibifu wa Vyakula na mali nyingine zilizokuwemo katika Nyumba hizo.

Kwa Upande wake Bi Aisha amesema kuwa, kutokana na Uharibifu huo ameguswa na hivyo ameahidi kuja kutoa msaada wa baadhi ya vitu kidogo vikiwemo vitabu vilivyo haribika ili kuwatia moyo na kuonyesha upendo na Ukaribu kwa wakazi hao wa Kata ya  Majohe.
Bi Aisha pamoja na Baadhi ya viongozi wa kata ya Majohe wakiangalia jinsi Upepo huo ulivyo athiri maeneo ya Kata hiyo

Hapa kulikuwa ni Makazi ya Mtu lakini Upepo umefanya paonekane kama ni Shamaba la kulimwa

Bi, Aisha Sururu akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo

No comments:

Post a Comment