Friday, March 15, 2013

ROBO FAINALI MABINGWA ULAYA: PSG KUIVAA BARCELONA


  Ratiba ya mechi za robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa leo mchana.

MONACO, Ufaransa

Aidha, ratiba ya michuano ya Europa League pia ilipangwa jana pia, ambapo Chelsea itatoana jasho na Rubin Kazan, Tottenham Hotspur itapimana ubabu na FC Basel Uswisi, huku Fenerbache ikicheza na Lazio nayo Benfica ikikipiga nma Newcastle.

HATIMAYE kitendawili cha mechi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kimeteguliwa leo mchana, baada ya kukamilika kwa tukio la upangaji ratiba, ambayo licha ya kuingiza timu tatu, klabu za Hispania zimefanikiwa kukwepana.

Katika ratiba hiyo, Malaga ya Hispania itaanzia nyumbani kuumana na Borussia Dortmund, kama itakavyokuwa kwa Real Madrid, iliyopangwa kukipiga na Galatasaray iliyo na nyota wa zamani wa Galacticos, Wesley Sneijder.

PSG ya Ufaransa itakuwa na kibarua kipevu kilichowashinda AC Milan, wakati watakapowaalika FC Barcelona ya Hispania, huku, Bayern Munich ya Ujerumani ikitarajia kutoana ngeu na ‘Kibibi Kizee’ Juventus Turin.

Mechi za robo faibali za michuano hii zinatarajia kupigwa Aprili 2 na 3, ambapo mechi kati ya Malaga dhidi ya Dortmund na ile ya Madrid na Galatasaray zitapigwa Jumanne Aprili 2, huku PSG dhidi ya Barca na ile ya Bayern na Juve itapigwa Jumatano Aprili 3.

Marudiano ya mechi hizo yatakuwa Apili 9 na 10, kusaka miamba minne itakayocheza nusu fainali ya michuano hiyo, itakayopigwa mwishoni wa mwezi ujao na kurudiana Mei mwanzoni, kusaka tiketi ya fainali Mei 25 kwenye Uwanja wa Wembley. 

Aidha, ratiba ya michuano ya Europa League pia ilipangwa leo katika hafla hiyo, ambapo Chelsea ya England itatoana jasho na Rubin Kazan ya Russia, huku Tottenham Hotspur ya England ikipimana ubabu na FC Basel Uswisi.

Fenerbache ya Uturuki itakuwa na kibarua dhidi ya SS Lazio ya Italia, huku Benfica ya Ureno ikikamuana na Newcastle ya England. Mechi za kwanza robo fainali hii zitapigwa Alhamisi ya Aprili 4 na marudiano yatakuwa Aprili 11.

No comments:

Post a Comment