Saturday, March 16, 2013

NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI AFUNGA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO


Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini , uliokuwa ukijadili Bajeti ya Mwaka 2013/2014, umefungwa jana  na  Naibu waziri wa Wizara hiyo Mhe Steven Maselle Katika Hoteli ya Bluer Pearl jijini Dar es Salaam.

Wakati akifunga, Mkutano huo, Mhe, Maselle amewapongeza wajumbe wa Baraza la mkutano huo kwa kuongeza mapato ya  Bajeti  kwa mwaka huu ambapo yamefikia wastani wa 75% tofauti na ilivyokuwa mwaka  jana  ambapo mapato yalikuwa chini ya asilimia 75%.
Amesema kuwa eneo la Madini ni moja ya  Sekta iliyofanikiwa kukuza Bajeti  ya mwaka huu kwani, wameongeza Mapato zaidi .

“Niwapongeze sana kwa kuwa Bajeti ya Wizara yetu sasa imekuwa tofauti na Wizara Zingine jambo ambalo linatupa faraja sisi viongozi hivyo endeleeni na Moyo huohuo wa kuweza kuhakikisha uchumi wa Tanzania Unakua kwa kasi.
Miongoni Mwa Agenda zilizo Zungumziwa katika kikao hicho ni pamoja na namna ya Kuboresha Utendaji wa Wizara, Namna ya kuhakikisha Uchumi wa Taifa unakua kwa kasi, na kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inapatikana ya uhakika ambapo  wamekubaliana kuwekeza katika  miundombinu ya Usafirishaji wa Umeme ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanafurahia Nishati ya umeme hapo Baadae.

No comments:

Post a Comment