Ugomvi dimbani: Mshambuliaji Fernando Torres wa Chelsea, akilalamikia
mbele ya mwamuzi baada ya kuchanika na kuanza kutokwa na damu kutokana
na kupigwa na mchezaji wa Steaua Bucharest. Chelsea ilishinda mechi hiyo
ya marudiano kwa mabao 3-1 na kufuzu robo fainali kwa jumla ya mabao
3-2.
Chukua hiyooo; Mshambuliaji Juan Mata wa Chelsea. Juu; akipiga shuti
kufunga bao la kwanza la timu yake. Chini; akishangilia bao hilo.
Hatari hapa, namna gani huyu; Raul Rasescu wa Bucharest (kulia), akiruka juu kujaribu kuwania mpira na David Luiz wa Chelsea.
Raha ya mechi bao; Wachezaji wa Chelsea wakishangilia bao.
Aaahhhh wapi!!!!! Mlinda mlango wa Chelsea, Petr Cech akishindwa kuzuia
shambulizi lililozaa bao pekee la Bucharest katika mechi hiyo.
Tunampenda/tunamuhitaji; Mashabiki wa The Blues wakimpigia chapuo la
mkataba mpya wa usajili kiungo-mchezeshaji wa timu yao, Frank Lampard.
Bao la ugenini; Wachezaji wa Bucharest wakishangilia bao ambalo liliwapa matumaini ya kusonga mbele.
Kisicho riziki, hakiliki; Furaha yao haikudunmu sanam, kwani bao la
Torres likatosha kuisukuma timu yao nje ya michuano, huku Chelsea
ikifuzu robo fainali Ulaya.
Nafunga kama hivi; Nahodha wa Chelsea, John Terry, akiruka juu kupiga kichwa kilichoipa timu yake bao la pili.
Chezea JT Wewee!!! Hapa Terry akishangilia bao lake.
Elininhooooooooo!!! Juu; Torres akipiga shuti kufunga bao la tatu la
Chelsea. Katikati; akishangilia bao hilo kwa kunyoosha mikono juu. Chini
akipongezwa na beki Ashley Cole.
No comments:
Post a Comment