Thursday, March 14, 2013

PROF, MUHONGO AMESEMA KUISHA KWA TATIZO LA UMEME KUNAHITAJI SUBIRA YA MIAKA MITATU MPAKA MITANO

 
Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo,amesema kuwa kuisha kwa tatizo la Umeme hapa nchini ni Ndoto zitakazotimia baadae sana kutokana na Serikali ya Tanzania kutokuwekeza kwenye Miundombinu ya Umeme kwa Zaidi ya Miaka Ishirini jambo ambalo linasababisha  Ugumu kwenye sekta ya Umeme hivi sasa kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linakwisha kwa haraka.

Ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutanowa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini uliofanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam.

Prof, Muhongo amesema kuwa, Kuhusu kukatika ovyo kwa Umeme Watanzania wavute Subira kwani sio jambo ambalo linaweza kufanyika kwa haraka hivyo Watanzania wametakiwa kusubiri kwa muda wa miaka mitatu mpaka Mitano.

Amezungumzia pia Swala la Gharama za Umeme na kusema kuwa, Gharama  hizo zitazidi kuwa juu kutokana na kwamba umeme unaotumika ni Umeme wa Mafuta tofauti na zamani ambapo ulikuwa unatumika umeme wa Mabwawa.

"Watanzania inabidi waendelee kuumia tu kwenye Gharama za umeme kwa kipindi cha miaka miwili, mpaka Ujenzi wa Bomba la Gesi utakapo kamilika ambapo Wananchi wataanza kutumia Umeme wa Gesi.", amesema Prof Muhongo.  
  
"Wananchi watakapo anza kutumia Umeme wa Gesi na ndipo Gharama za Umeme zitakaposhuka", ameongeza.

Prof Muhongo amewataka Wajumbe wa Kikao cha Baraza la Wizara ya Nishati na Madini kujadili namna ya Kuboresha Utendaji wa Wizara pamoja na Kuhakikisha kuwa Uchumi wa Tanzania Unakua kwa kasi zaidi.

Aidha amewataka pia kujadili namna Tanzania itakavyojenga uchumi ambao unampa matumaini maskini na juu ya namna Umeme wa uhakika utakavyopatikana. 

No comments:

Post a Comment