Monday, March 4, 2013

MUUNDO MPYA WA MISHAHARA YA KENYA UTAANZA BAADA YA UCHAGUZI WA LEO


Tume ya Mishahara na Malipo ya Kenya (SRC) imetangaza muundo wa malipo ya mwisho kwa viongozi wa serikali ambao utaanza kutumika baada ya uchaguzi wa LEO.
Chini ya muundo huo mpya wa malipo, rais atapokea mshahara wa mwezi wa shilingi milioni 1.24 (dola 14,400), uliopunguzwa kutoka shilingi milioni 2 (dola 23,300) ambazo Rais Mwai Kibaki alikuwa akipokea.
Magavana watapokea shilingi 640,000 (dola 7,450) kwa mwezi, na wabunge watapokea shilingi 535,000 (dola 6,230), zilizopunguzwa kutoka shilingi 851,000 (dola 9,910).
Utaratibu mpya wa malipo umezingatia kurekebishwa kwa malipo ya viongozi ambayo tume iliwasilisha kwa umma tarehe 5 Februari. Madai ya malipo kwa sekta ya umma kwa sasa ni zaidi ya asilimia 30 ya bajeti ya taifa, iliyosababisha uchunguzi wa hali ya juu.
"Madai yaliyopo ya malipo hayalipiki wala hayaendelezeki," alisema mwenyekiti wa SRC Sarah Serem. "Nchi imevuka mbali lengo la bajeti na kukua kwa uchumi kama vile uendelevu wa kifedha."

No comments:

Post a Comment