Mahakama ya rufaa ya Somalia siku ya Jumapili (tarehe 3 Machi) ilfuta mashtaka dhidi ya mwanamke aliyehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja baada ya kumwambia mwandishi wa habari kuwa alibakwa na vikosi vya usalama, lakini mwandishi wa habari ataendelea kubakia jela, AFP iliripoti.
"Mahakama hiyo iliamuru kuachiwa huru
mwanamke huyo, huku mwandishi wa habari atabakia jela kwa miezi sita kwa
kukosea taasisi za serikali," Jaji Hassan Mohamed Ali alisema.
"Mahakama imejua kuwa mwandishi wa habari alimdanganya mshtakiwa
anayedaiwa kubakwa ili kufanya mahojiano."
Mwezi uliopita, mwanamke, Lul Ali Osman, na mwandishi wa habari
Abdiasis Abdinuur Ibrahim, mwenye umri wa miaka 25, walipatikana na
hatia ya kukosea taasisi za serikali. Ibrahim pia alipatikana na kosa la
"kufanya mahojiano ya uongo, na kuingia kwenye nyumba ya mwanamke huyo
ambaye mumewe hakuwepo".
Osman, ambaye mwanzoni alitakiwa kukaa kwa miezi sita bila
kumnyonyesha mwanaye mdogo kabla ya kuanza kutumikia kifungo chake cha
jela, aliachiwa huru kutoka katika mahakama ya Mogadishu baada ya uamuzi
huo kutolewa.
Lakini Ibrahim alifungwa pingu na kuingizwa kwenye lori
lililomrudisha gereza kuu, kulikochochea majibizano ya hasira kutoka
kwenye vikundi vya haki na wenzake.
Daniel Bekele, Mkurugenzi wa Afrika wa shirika la haki za binadamu la
Human Rights Watch, alikosoa kuendelea kumtia ndani Ibrahim, ambaye
amekuwa jela kutoka tarehe 10 Januari.
"Mahakama ya rufaa ilipoteza nafasi ya kufanyia haki kosa la kutisha,
kwa mwandishi wa habari pamoja na kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini
Somalia," Bekele alisema katika taarifa. "Serikali imetoa wito kwa
mahakama kuweka uelekeo wake katika kesi hii, lakini kila hatua haki
imekiukwa"
No comments:
Post a Comment