Watu wasiopungua watatu waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa siku ya
Ijumaa (tarehe 1 Machi) katika mashambulio mawili kwenye mgahawa ulio
katika fukwe za mbele maarufu huko Mogadishu, AFP iliripoti.
Milipuko hiyo iliripotiwa kusababishwa na
washambuliaji wa kujitoa muhanga waliovaa fulana zilizosheheni milipuko,
ikifuatiwa na bomu la gari.
"Mwanaume huyo alijilipua wakati walinzi wa lango la mgahawa
walipokuwa wakijaribu kumzuia… takriban watu watatu pamoja na mlipuaji
walikufa," alisema Hersi Adan, kiongozi wa usalama ambaye alikuwepo
karibu na tukio la shambulizi.
"Dakika chache baadaye gari liliegeshwa nje ya jengo hilo lililipuka na kuua mwingine na kujeruhi watu saba," alisema.
Mlipuko huo ulitokea karibu na ufukwe maarufu wa Lido huko Mogadishu,
ambao kwa kawaida hujaa watu siku za wikendi pamoja na familia
zikifurahia ufukwe, kucheza mpira wa miguu au kuogelea katika Mawimbi ya
Bahari ya Hindi.
Hakuna kikundi kilichodai kwa haraka kuhusika na mlipuko huo, lakini
al-Shabaab imezindua mfululizo wa mashambulizi ya mtindo wa vita vya
msituni huko Mogadishu katika miezi ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment