Monday, March 4, 2013

MAMA TUNU PINDA ANOGESHA HAFLA YA WOMEN'S CELEBRATION 2013

 
Mwandaaji wa hafla ya Women's Celebration 2013 kutoka kampuni ya 8020 Fashions Blog, Shamim Mwasha akipongezwa na Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwa kazi nzuri alioifanya ya kufanikiwa kuwakusanya wanawake wenzake na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na maendeleo kwa ujumla,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi 8 Duniani kote.
Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akisoma hotuba fupi mbele ya wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions Blog,iliofayika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni mwelekeo wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimisha Machi 8 Duniani kote.
 Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akisalimiana na mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwenye hafla ya Women's Celebration 2013 iliofanyika leo jijini Dar.
 Mwanamuziki mwimbaji mahiri wa miondoko ya taarab,Khadija Kopa akitumbuiza mbele ya wageni waliohudhuria hafla ya  wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions Blog,iliofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.
 
 Mke wa waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (pichani katikati) akijimwaya mwaya pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
 Naibu Waziri wa Sheria na katiba,Mh. Angellah Kairuki akiwa sambamba na Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Mmoja wa washiriki wa hafla hiyo akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakifutailia mambo yaliyokuwwa yakijiri ukumbini humo.

No comments:

Post a Comment