Katibu
wa Bunge Ndg. John Joel akitangaza Matokeo ya wenyeviti na Makamu wa
Wenyeviti mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi hao katika
kamati zote za Bunge leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa kamati za Bunge
Ndg. Theonist Luhirabake na kulia ni Afisa Habari wa Bunge Ndg. Owen
MwandumbyaWajumbe wa Kamati ya PAC wakiteta na Mhe. John Cheyo anaye tetea kiti chake cha uenyekiti wa kamati Mhe.
David Kafulila akimpongeza Mhe. James Lembeli mara baada ya kupita bila
kupingwa kwa nafasi ya uenyekiti wa kamati ya Ardhi Maliasili na
Mazingira
.
Msimamizi wa Uchaguzi katika kamati ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa
kimataifa Bi. Justina Shauri akiwapa maelezo ya awali wajumbe wa kamati
hiyo kabla ya kuchagua viongozi wao. Msimamizi
wa Uchaguzi katika kamati ya Ulinzi na Usalama Ndg. Peter Magati
akiwapa maelezo ya awali wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuchagua
viongozi wao.
Katibu
wa Kamati ya PAC Bi. Lina Kitosi ambaye pia ndiye msimamizi wa uchaguzi
akiwaonesha wajumbe wa kamati hiyo karatasi maalum ya kupigia kula
kabla ya uchaguzi kufanyika
Mgombea
nafasi ya Uwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto
Kabwe akinadi sera zake mbele ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya
kufanyika kwa uchaguzi leo
Mgombea wa Nafasi ya Uenyekiti katika kamati ya LAAC Mchungaji Israel Natse nae akinadi sera zake
No comments:
Post a Comment