Thursday, March 14, 2013

KESI YA MWANGOSI YAZIDI KUPIGWA DANADANA 
 Mtuhumiwa wa mauwaji ya  Mwangosi  akifichwa na askari kanzu  leo
 Hivi ndivyo askari  kanzu  walivyojaribu kumficha mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi leo
Huyu  ndie mtuhumiwa wa mauawaji ya Mwangosi (kulia)
UPELELEZI  wa  kesi  mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa chanel ten mkoani
Iringa, marehemu Daud Mwangosi umeendelea  kupingwa  dana dana baada  ya  upande  wa jamhuri
kuomba  kesi hiyo ipangiwe  tarehe  nyingine ya kutajwa kutokana na upelelezi  wake 
kutokamilika .

Katika  kesi hiyo ambayo mtuhumiwa  wake ni  askari  wa  kikosi  cha kutuliza ghasia mkoa  wa Iringa
(FFU) Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G 2573
Leo alifikishwa mahakamani hapo huku mkuu  wa  polisi wilaya (OCD) akiwazuia askari kuwazuia wanahabari kutimiza  wajibu  wao
Akisoma kesi hiyo mbele ya mwendesha mashitaka Adolf Maganga, hakimu
mkazi mwandamizi mfawidhi  wa  mkoa  Juma Hassan alisema kuwa upelelezi bado haujakamilika
hivyo unahitajika muda zaidi kwa ajili ya uchunguzi wa kesi hiyo ya
mauaji.

Mtuhumiwa  Simon alifikishwa mahakamani hapo tofauti na
ilivyokuwa  alipofikishwa kipindi kilichopita ambapo leo  alikuwa na
askari kanzu wawili tu ambao  walikuwa  wakifanya jitihada za kumficha ili asipigwe  picha

Kesi hiyo itasomwa tena Machi 28,mwaka huu ambapo mtuhumiwa
amerudishwa mahabusu.

Awali Februari 28, mwaka huu mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani na
kusomewa kesi yake ”Chamber court”ambako waandishi wa habari
hawakuruhusiwa kuingia wala kusogea karibu eneo la chumba kilichokuwa
kikisomewa kesi.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo akiwa amezungukwa na askari
kanzu wengi kama mahabusu wakilenga kukomesha waandishi wa habari
wasipate picha mtuhumiwa huyo.
Akifikishwa mahakamani hapo, mtuhumiwa huyo alikuwa katika gari la
mahabusu (karandinga) kama watuhumiwa wengine tofauti na siku za
mwanzo alipokuwa akifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari.


Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la
kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO
huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani
hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku
waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika
kupigwa jambo lililoamsha hisia tofauti miongon

Katika hali isiyo ya kawaida, 14 Februari Mwaka huu mtuhumiwa huyo
mwenye namba G 2573 akiwa mahakamani hapo aliwatukana waandishi wa
habari matusi ya nguoni kuwataka wasimpige picha huku akijidai kuwa
muda si mrefu ataachiwa na kupambana na waandishi mitaani.

Siku hiyo(Februari 14,2012) Pasificus akiwa na jazba alisikika akisema
“mtapiga picha sana mtakavyo lakini hamjui kama kesho tu nitatoka
halafu tupambane mitaani huko. Nawaona sana mnaonipiga picha tutakuja
kukutana tu” alisema mtuhumiwa huyo.


Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka jana katika kijiji cha
Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari
wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).

No comments:

Post a Comment