Thursday, March 14, 2013

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa UAE Nchini Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Al Suwaidi. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisi kwa Mhe. Waziri Membe leo tarehe 14 Machi, 2013.
 Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Balozi Al Suwaidi  masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na UAE mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi huyo.
Mhe. Balozi Al Suwaidi akichangia hoja wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Membe. Mwingine katika picha ni Bw. Hangi Mgaka, Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Mashariki ya Kati.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

No comments:

Post a Comment