Vyuo vikuu nchini Tanzania vimeshauriwa kuhakikisha
vinajitanua kimataifa katika kutoa elimu yake jambo ambalo limetajwa kuwa
litasaidia wanafunzi wa Tanzania kujifunza mambo mapya katika nchi nyingine.
Hayo yamesemwa leo na mkuu wa chuo kikuu huria cha Tanzania Prf TOLLY MBWETTE wakati akisaini mkataba wa makubalioano ya ushirikiano na
serikali ya Namibia kupitia chuo chake cha TRIUMPHANT
COLLEGE mkataba wenye malengo ya
kushirikiana kitaaluma baina ya vyuo hivyo viwili.
Prof, MBWTTE
amesema kujitanua kimataifa ni jambo muhimu ambalo amesema moja kati ya faida
zake kubwa ni kusaidia wanafunzi kupata elimu bora na yenye viwango vya
kimataifa zaidi.
Aidha amesema chuo kikuu huria kimekuwa ni chuo kikuu cha
kwanza kusaini mkataba wa kimataifa wa kusaidia katika elimu jambo ambalo
amesema liafaa kuigwa kwa vyuo vingine ili visaidie katika kukuza elimu ya
Tanzania.
No comments:
Post a Comment