Wednesday, March 13, 2013

BARCELONA YAICHAPA AC MILAN 4-0 NA KUINGOA MABINGWA ULAYA

 Dimba la Nou Camp dakika chache kabla ya wenyeji FC Barcelona kukipiga na AC Milan, katika mechi ya marudiano mtoano wa 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo Barca ilishinda kwa mabao 4-0 na kuing'oa Milan kwa jumla ya mabao 4-2.
 Lionel Messi akishangilia bao la kwanza la Barcelona, kama ubao unavyosomeka hapo juu.
 Gerrard Pique katikati akishangilia bao la pili lililofungwa na Messi (10), sambamba na wachezaji wa FC Barcelona.
 Hapa Messi akipenyeza shuti kufunga moja ya mabao yake mawili katika ushindi wa Barca wa mabao 4-0. Licha ya kukabwa na mabeki msitu kama inavyoonekana, lakini haikuwa sababu ya Muargentina huyu kutotisha dimbani kama ilivyo kawaida yake.
 Mlinda mlango wa AC Milan Christian Abbiati, akiruka juu kupangua shuti.
 Messi akishangilia bao lake.
 Andres Iniesta akishangilia akiruka kushangilia moja ya mabao ya Barcelona dhidi ya AC Milan.
 Ulinzi wa kutosha alipewa kama inavyothibitisha picha hii hapa, Messi akichuana na mabeki wa AC Milan, lakini alikuwa moto wa kuotea mbali akifunga mara mbili.
 David Villa akiifungia Barca bao
  Mlinda mlango wa Milan, Abbiati, akijaribu bila mafanikio kuzuia shuti la Villa lisitinge nyavuni.
 Ilikuwa ni furaha isiyopimika kwa wachezaji wa Barca, huku wale wa Milan wakishindwa kuamini kilichotokea.
Furaha ya ushindi mbele ya mashabiki.

No comments:

Post a Comment