Wednesday, March 13, 2013

MKURUGENZI WA NEPAD AFANYA ZIARA TFDA MAPEMA LEO

Bango Maalum Kwa ajili ya Kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa (NEPAD) Alipo fanya Ziara yake  leo katika Mamlaka ya Chakul;a na Dawa (TFDA)
 
Mamlaka ya chakula na Dawa  TFDA imetembelewa na Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi  iliyopo chini ya  Umoja wa Africa New Partnership for Africa’s Development  Agency  (NEPAD) Dr, Ibrahim Assane Mayaki ambapo amesema kuwa   amefurahishwa  na  Utendaji kazi wa TFDA katika Udhibiti wa Chakula na Dawa.
Dr  Mayaki  ameisisitiza TFDA kuwa na ushirikiano wa pamoja Africa nzima ili wawe na mtazamo unaofanana ili kuweza kuboresha Bidhaa zote za Afrika kwa ujumla katika Kiwango cha Kimataifa.
“Tunataka  Africa iwe na Mtazamo unaofanana ili kama bidhaa ikliwa haina kiwango cha  ubora basi bidhaa hiyo ikataliwe Africa nzima,”  amesema Dr Mayaki.
Aidha Dr Mayaki ameonyesha  kufurahishwa na Maabara ya TFDA ambapo amesema kuwa  ni Maabara  yenye kiwango  kinacho kubalika kimataifa.
Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi  iliyopo chini ya  Umoja wa Africa New Partnership for Africa’s Development  Agency  (NEPAD) Dr, Ibrahim Assane Mayaki  Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao makuu ya Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA alipotembelea katika Ziara yake aliyoifanya TFDA mapema leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA  Bw, Hiiti Sillo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA akimkabidhi Zawadi maalum Dr, Mayaki kama ishara ya Kumpongeza kwa  kufanya Ziara yake TFDA

Mayaki yupo Makini kuongea na waandishi wa habari

Wafanyakazi wa TFDA wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Dr Mayaki

No comments:

Post a Comment