Monday, March 18, 2013

ASKARI WA USALAMA BARABARANI AGONGWA NA GARI MPAKA KUFA NI BAADA YA MSAFARA WA RAIS KUPITA

Akizungumza na WAPO Radio FM kwa njia ya simu akiwa katika hospitali ya Muhimbili, Kamanda wa Kipolisi kwa mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela amesema marehemu WP2492 Koplo, Elikiza Nnko wa Usalama wa Barabarani, baada ya kupewa taarifa kuwa magari ya msafafa wa Rais yameshapita yote, alirudi barabarani ili kuongoza magari mengine pasipo kujua kuwa dereva mwenye gari Landrover Discovery lenye namba za usajili T328BML mali ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), alipoona msafara umepita, kwa kasi alichomoa gari na kutaka kuiunga ionekane kuwa ipo kwenye msafara wa Rais ili apate kupita kwa urahisi, na ndipo aliposababisha ajali na kifo na kisha kutoroka kuelekea maeneo ya Ubungo na kujichanganya na magari mengine. Jeshi la polisi limeshachukua hatua ya kuwasiliana na viongozi wa TAG ili kumpata mhusika.

Bofya kifute cha pleya hapo kuisikiliza taarifa hiyo.


Mchana wa leo tovuti ya GPL imeripoti tukio la kusikitisha la kifo cha Askari Polisi wa usalama Barabarani, aliyetambulika kwa jina la Elikiza (pichani juu, bofya kuona picha iliyofichwa nyuma yake), baada ya kugongwa na gari katika eneo la Bamaga, Sinza jijini Dar es Salaam.

Maelezo ya WillyIAm (
via JF) yanayofuatia picha yanatoa taarifa zaidi:
Picture
(Picha na Shauri Kati / GPL)
Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.

Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:

Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayo-cross from Shekilango.

Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.

Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.

Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu

No comments:

Post a Comment