Monday, March 18, 2013

LWAKATARE NA JOSEPH LODUVICK WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Picture
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare, akionyesha vidole viwili huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wakati alipofikishwa kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo anayeonekana nyuma yake liyevalia nguo nyeusi ni Joseph Ludovick anayedaiwa kurekodi video ya Lwakatare ya njama za Kuwadhuru waandishi wa Habari. (picha: Mzuka wa Fungo blog)

Picture
Ludovick akionyesha Ishara ya Vidole viwili ikiashiria anaunga Mkono CHADEMA wakati akipelekwa Mahakamani.
Picture
(picha: Mzuka wa Fungo blog)


Imeandikwa na Happiness Katabazi (via blog)

HATIMAYE Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Dk Eliezer Feleshi amemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na mwenzake kwa makosa ya ugaidi.

Mbali na Lwakatare mshitakiwa mwingine ni Ludovick Rwezaula Joseph ambao wanatetewa na mawakili wa kujitetemea Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Nyaronyo Kicheere.

Washitakiwa hao wakifikishwa saa mbili asubuhi mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ilala, Duwani Nyanda na kuhifadhiwa nyuma ya jengo la mahakama hiyo tayari kwa ajili ya kufikishwa kizimbani kosomewa mashitaka yanayowakabili.

Washitakiwa hao waliingizwa ndani ya ukumbi namba moja wa mahakama hiyo saa 7:06 mchana chini ya ulinzi mkali wa wanausalama, huku Lwakatare akiwasalimu wafuasi wa CHADEMA kwa kuwaonyesha ishara ya vidole viwili ambapo wafuasi hao walikuokuwa wamefurika mahakamani hapo tangu asubuhi, wakimjibu kwa kumuonyeshea ishara ya

No comments:

Post a Comment