Thursday, March 28, 2013

AJALI MBAYA YATOKEA JIJINI DAR,, YASADIKIKA WATU ZAIDI YA WATANO WAFARIKI PAPO HAPO

Lori lililo sababisha Ajali maeneo ya Tabata Relini jijini Dar es Salaam baada ya Kuacha Njia na kuhamia upande wa pili na kugonga watu pamoja na Magari. Ajali hiyo ilihusisha Magari Madogo, Bajaji, Pikipiki aina ya Bodaboda na pia iliwagonga watembea kwa Miguu.
 Kwa mujibu wa Mashuhuda wa Ajali hiyo iliyotokea usiku huu, wamesema kuwa Magari yaliyogongwa yalikuwa yanasubiri kuruhusiwa na taa ili waweze kupita ndipo Lori  hilo la Kampuni ya ASAS kutoka Tanga Tanzania, lilipo acha njia na kuhamia upande wa pili,.
Gari lenyewe hili hapa

Piki piki pamoja na Dereva wake wakiwa wamekandamizwa na Gari hilo

Ni mali ya Kampuni ya ASAS kutoka Tanga Tanzania
Picha zote na Maasinda blog

No comments:

Post a Comment