Changamoto ya
uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo,
ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.
Hizi ni aina
ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa
ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za
ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.
Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji wakijitahidi kuwanasua watu kwenye kifusi.
Hapa watu wamo ndani ya Kifusi hiki |
Waziri wa
Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka
kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova
kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi
katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha
Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote
na Habari Mseto Blog)
No comments:
Post a Comment