Juzi, vyombo vya habari viliripoti kuhusu, “Mwanamke albino anyofolewa mkono”. Taarifa mpya zilizopatikana kama zinavyoonekana pichani, ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya (wa tatu kulia) akibubujikwa na machozi jana usiku hali akushuhudia Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Peter Ngusa (kulia) akiwa ameushikilia mkono ulionyofolewa hivi karibuni kutoka kwa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa porini kijijini Miangalua wilayani Sumbawanga. Hapa chini, anauonesha hadharani mbele ya majengo ya Hospitali ya Mkoa mjini hapa, watatu kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk John Gurisha. |
Mmoja wa askari akifungua majani ya mgomba yaliyoufunga mkono ulionyofolewa hivi karibuni kutoka kwa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa poroni kijijini Miangalua wilayani Sumbawanga ambao akiuonesha hadharani mbele ya majengo ya Hospitali ya Mkoa mjini hapa jana usiku jana Februari 14. |
No comments:
Post a Comment