Friday, February 15, 2013

JUKWAA LA KATIBA LAPINGA VIKALI MADIWANI KUWEKWA KATIKA UJUMBE WA MABARAZA NGAZI YA WILAYA KWA NYADHIFA ZAO

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo katika Mkutano uliofanyika katika makao makuu ya Jukwaa hilo.
 Jukwaa la Katiba Tanzania leo limeitaka Tume ya Katiba kutowaweka Madiwani kuwa wajumbe wa moja kwa moja kwa nyadhifa zao katika Baraza la Katiba Ngazi ya Wilaya.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Bw Deus Kibamba amesema kuwa, hawaoni umuhimu wa Madiwani kuwekwa kwenye Ujumbe kwa nyadhifa zao kwani wao walichaguliwa kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi katika ngazi ya Mabaraza ya Madiwani ya Wilaya, Manispaa, Jiji na vijiji na sio katika Mabaraza ya Katiba.

Amesema kuwa, kuwahusisha madiwani kutasababisha mgogoro wa itakadi za vyama vilivyo waweka Madiwani hao Madarakani.

Bw, Kimamba amesema kuwa wanapendekeza wajumbe watakao chaguliwa kwenye Mabaraza ya Katiba kuwa na sifa ya kuwa Mtanzania aliyezaliwa Tanzania na sio raia wa Kuandikishwa, na pia awe ni  Mkazi wa Kudumu wa Mahali husika.
Wadau pamoja na waandishi wa habari walio hudhuria katika Mkutano huo wakisikiliza kwa makini

No comments:

Post a Comment