Dr, Joseph Odumodu Mkurugenzi TBS Nigeria |
Akizungumza katika mahojiano wakati wa mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la viwango Tanzania TBS yaliyopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Shirika la viwango nchini Nigeria Dkt, Joseph Odomudu, amesema kuwa lengo lao la kufanya ziara Nchini Tanzania ni kwa ajili ya kujenga mahusiano mazuri baina ya nchi hizo ambazo ni Tanzania na Nigeria.
Dkt, Odumodu amesema kuwa, wamefurahishwa na utendaji mzuri wa kazi unaofanywa na Shirika la viwango la Tanzania na kuongeza kuwa endapo TBS Tanzania itashirikiana vizuri na TBS Nigeria kutakuza bihashara na bidhaa za kiafrika kwani zita aminika kila mahali Afrika na hata Mabara mengine.
"Niwakati wetu sasa sisi wa Afrika wote kufanya kazi kama kikundi kimoja kwa pamoja ili tuweze kukuza bihashara zetu na kutambulisha bihashara zetu mbali zaidi", amesema Dkt, Odumodu.
Bw, Leandri S Kinabo Kaimu Mkurugenzi TBS Tanzania |
No comments:
Post a Comment