KASI ya maendeleo Wilayani Kilwa inatarajiwa kuongezeka kuanzia sasa
baada ya Makampuni manne ya Kimataifa kuwekeza vitega uchumi Wilayani humo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo Adoh Mapunda alisema halmashauri yake kwa sasa imezipokea kampuni
nne za wawekezaji wapya wa kimataifa ambao wataongeza ajira kwa wakazi wa Kilwa
na Tanzania kwa ujumla.
Mapunda aliyataja makampuni hayo na
kiwango cha ajira kitakachotokana na makampuni hayo pamoja na hali ya kiuchumi
itakavyokua kwa kasi.
Statoil Tanzania Ltd kutoka nchini
Norway ambayo imegundua gesi na inatarajia kujenga mtambo mkubwa wa kuchakata
gesi (Liquidified natural gas) kwenye kata ya Lihmalyao kwa gharama ya Tsh18Billioni
na kutoa ajira zaidi ya 16,000.
Kampuni nyingine ni Kilwa Energy Tanzania Ltd,
itakayofua umeme na kuingiza kwenye gridi ya taifa kuanzia kwenye eneo la
Somanga hadi Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo inatarajiwa kuzalisha
ajira za zaidi ya 800.
Kampuni nyingine ni ile ambayo
imeshaanza uzalishaji kwenye eneo hilo la Kilwa ni ya Lee Cement Factory ambayo
inatengeneza Saruji mjini Kilwa na kusababisha bei ya saruji Wilayani humo
kushuka kutoka Tsh 18,000 hadi 13,000 ambapo kiwanda hicho kinauwezo
wakutengeneza tani 8334 kwa mwezi.
Kampuni nyingine aliitaja kuwa ni Kaidi
kutoka nchini China ambayo inawekeza kwenye kilimo na imepewa eneo la Ekari
13,000 kwenye vijiji vya Mitole na Ngea, ambako kutalimwa mazao mchanganyiko
yakiwamo Mpunga, Mahindi, Mihogo, Miwa Mtama na matunda. Mbali na kilimo
kampuni hiyo pia itazalisha umeme utakaotokana na takataka.
Adoh alisema halmashauri imeshapokea
Tsh200Millioni ikiwa ni sehemu ya asilimia0.3 kutoka kwa kampuni ya kampuni ya
gesi, ushuru wa Tsh200,000 unaotokana na
madini ya jasi yanayotengenezwa saruji.
Vyanzo hivyo vya pesa vitasaidia sana
kuinua maendeleo Wilayani humo.
No comments:
Post a Comment