Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh, Yusuph Mwenda, amemtaka Mbunge wa Jimbo la Kawe Mh Halima Mdee kujiunga katika Chama Cha Mapiduzi ili waje wafanye kazi kwa pamoja ndani ya Chama hicho.
Ameyasema hayo leo katika mkutano wa Kuzindua Daraja la Mtaa wa Ndumbwi kata ya Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya amesema kuwa anamkubali sana Mbunge Mdee kwa Utendaji kazi wake kwani ni mchapa kazi mzuri katika Jimbo lake.
“Jamani Viongozi wa Chama jaribuni kumshawishi Mhe, Mbunge wetu wa jimbo la Kawe Halima Mdee ili arudi kwenye Chama cha Mapinduzi tuungane tufanye kazi kwa pamoja”, amesema Mwenda.
Meya pia amewataka wananchi wa Mbezi Juu kusimamia Ujenzi wa Daraja linalojengwa Mbezi Juu Mtaa Ndumbwi na kuhakikisha kuwa linajengwa kwa viwango bora.
No comments:
Post a Comment